Biashara vyuma chakavu imulikwe

Niliandika barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kwamba biashara ya chuma chakavu inafanyika bila leseni, inakwepa kodi, inahujumu miundombinu, inahodhiwa na wageni, inatakatisha fedha chafu, lakini hatua hazijachukuliwa. Ninazidi kuomba chama tawala kitupie jicho kero hii. Haki na amani ni mapacha, na tanzania ni yetu sote.

 

H.Q. Batamuzi

0782 828 856

Je, hii ni sahihi kwa rais?

Nimesikitishwa na kaulia ya Rais Kikwete wiki iliyopita, nilipokuwa ninaangalia ziara yake nchini Japan. Alikuwa anaongea na Watanzania waishio Japan kuhusiana na udini hapa nchini na wao wakaeleza wanavyoshangaa kuhusu vuguvugu la udini nchini. jinsi wanavyoshangaa ndivyo na Rais Kikwete anavyoshangaa. Je, hii ni sahihi kwa rais?

 

0752 633 555

 

Tanesco Kyela kero tupu

Mteja wa Shirika la Taifa la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) amelipa gharama za kuunganishiwa mita mpya ya umeme mahali ambapo hapahitaji nguzo, lakini tangu mwezi Mei mwaka huu, hajaunganishiwa na hajaambiwa kilichokwamisha mpango huo! Hivi kweli ni hii halali, inawezekana?

 

Msomaji Kyela, Mbeya

0767 529 747

 

Serikali ya CCM vipi?

Badala ya kutekeleza ahadi yake ya kuboresha maisha bora kwa kila Mtanzania, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inatukamua kwa kututoza kadi ya simu za mkononi! Si ajabu itaanza kututoza pia kodi za vikokotozi na saa za mkononi! Hali hii itawafanya Watanzania wengi kuwa mafukara zaidi!

 

Paschal Mtalima, Sumbawanga

0688 702 268

 

Ninamuunga mkono Balile

Ninakubaliana  na ndugu [Deodatus] Balile kwamba si vizuri vyama vya siasa kuwa na majeshi, lakini tatizo la Tanzania ni wale waliopewa dhamana ya kusimamia serikali kukipendelea CCM na kukandamiza vyama vya upinzani. Hivi inaingiaje akilini kuwa ‘Green Guards’ kwa CCM ni ruksa lakini ‘Red Brigade’ kwa Chadema ni kosa?

 

Kimaro GJ, Dodoma

0715 581 952

 

Spika Makinda anapwaya

Ni ukweli ulio wazi kwamba kiti cha Spika kinachoongozwa na mama [Anne] Makinda kimepwaya katika kuisimamia serikali na kulinda maslahi ya Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao. Kuwe na kanuni inayotamka wazi kwamba kama Spika atatoka chama tawala, basi naibu wake atoke chama cha upinzani.

 

Boniface Kimambo

0714 100 756

 

Tunahitaji watu kama Manyerere

Ninampongeza mwandishi wa makala iliyopo safu ya Jamhuri ya Waungwana [Manyerere Jackton], kwenye Gazeti la Jamhuri la Julai 16-22, 2013. Uchambuzi wake ni makini, wa kisomi, wenye ‘evidence’. Watanzania uzalendo kwa taifa haupo, viongozi hawajali maslahi ya wote, wachache wanajinufaisha. Wasomi kama nyie mmetumiwa vipi kufanya tafiti bora za taifa?

 

bonnietheos@yahoo.com

 

Kutukanwa kwa rais mh!

Namuunga mkono Manyerere Jackton kwa maelezo yake mengine, lakini nina mtazamo tofauti kabisa na yeye kuhusu kutukanwa kwa Rais Kikwete. Marekani wanaandamana kwa kosa la kuuawa mtu mmoja na mtuhumiwa kuachiwa. Kuna Watanzania wangapi wameuawa na kusababishiwa vilema na vyombo vya dola? Serikali ya CCM haiwezi kukwepa lawama.


Magambo

0787 031 994

1209 Total Views 3 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!