Kimahesabu Argentina Ishatoka kwenye Hatua ya Makundi Kombe la Dunia

Kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kimeshindwa kutamba mbele ya Croatia baada ya kukumbana na kichapo cha mabao 3-0.

Mabao ya mchezo huo wa kundi D yaliwekwa kimiani na Luca Modric, Ivan Rakitic na Ante Rebic.

Kufuatia kichapo hicho walichokipata Argentina kinawafanya wasalie na alama moja waliyoipata dhidi ya Iceland baada ya kwenda sare ya 1-1 wakiwa nafasi ya 3.

Nyota wa timu hiyo, Lionel Messi alionekana kuwa na machungu kufuatia kichapo hicho ambacho ni kama dhamaha kubwa kwake.

Messi ambaye amepewa nafasi kubwa zaidi ya kuisaidia Argentina ameshindwa kufunga bao lolote mpaka sasa katika michezo miwili ambayo timu hiyo imeshacheza.

1396 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!

Comments

comments

Show Buttons
Hide Buttons