Ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Msanii wa Bongo Movie, Elizabeth Michael maarufu kwa jina lake la sanaa la Lulu ambaye anatumikia kifungo chake gerezani, ametumia siku ya leo kutoa zawadi kwa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Lulu ambaye anatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kosa la kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika hafla ya utoaji zawadi hizo amewakilishwa na Mama yake mzazi, mwigizaji mwenzake, Dr Cheni pamoja na marafiki zake mbalimbali.

Katika ujumbe wake, Lulu amesema kuwa, anawapenda sana, anawaombea watoto hao na kuwa anaamini wakiwa huru na kumuomba Mungu basi haya maradhi yatakuwa ya muda mfupi na afya za watoto zitakuwa nzuri.

Lulu mwenye umri wa miaka 23 sasa, alizaliwa Aprili 16, 1995 jijini Dar es Salaam na kulelewa na wazazi wake, Michael Kimemeta na Lucrecia Kalugira.

Hapa chini ni picha za watoto hao wakipewa zawadi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.

 

 

2632 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!