Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kukagua hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu mjini Dodoma.

Komando wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakionesha umahiri wao wakati wa maandalizi ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu mjini Dodoma.

Askari wa Jeshi la Magereza, wakionesha zoezi la kupambana na adui mbele Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018.

Mwanamuziki mkongwe hapa nchini Bw. Cosmas Chidumule akitumbuiza kama sehemu ya maandalizi ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu mjini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri mjini humo.

Wanafunzi wanaounda kikundi cha halaiki wakionesha umahiri wao katika kupambana na adui wakati wa maandalizi ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu mjini Dodoma.

Kikosi cha Komando wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakionesha umahiri wao katika kupambana na adui.

Wanafunzi wanaounda kikundi cha halaiki wakionesha uwezo wao katika kupambana na adui wakati wa maandalizi ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu mjini Dodoma. ( Picha zote na Idara ya Habari MAELEZO).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Ameyasema hayo Jumanne, Aprili 24, 2018 mara baada ya kukagua maandalizi hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ambapo amesema maandalizi yanaendelea vizuri.

Waziri Mkuu amejionea maonesho mbalimbali yakiwemo ya kikundi cha halaiki ambacho kinaundwa na wanafunzi 2,000 kutoka Manispaa ya Dodoma pamoja na maonyesho ya kujihami na maadui yaliyooneshwa na Jeshi la Magereza.

“Nimeridhika na kazi ambayo mmeifanya, nawaruhusu muendelee kushirikiana katika kukamilisha maeneo ambayo yamesalia na kuanzia kesho tujiandae kuwapokea wageni kutoka maeneo mbalimbali.”

Alhamisi Aprili 26, 2018 Watanzania wanatarajia kuadhimisha miaka 54 ya Muungano tangu Tanganyika ilipoungana na Zanzibar, chini ya waasisi wake Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

41193 – DODOMA.

JUMANNE, APRILI 24, 2018.

By Jamhuri