MAKAMU wa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Pemba, Ali Mohammed Ali, ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa huo.

Makamu huyo ameungana na Rais wa chama hicho, Ravia Idarous Faina, Makamu wa Rais Unguja, Mzee Zamu Ali na Abdul Ghani Msoma.

Akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba, makamu huyo alisema hatua hiyo imekuja baada ya kujitathmini kwa kina na kuona tayari viongozi wenzake wameshaachia nyadhifa zao.

“Baada ya kuona viongozi wenzangu wa juu wamejiuzulu nyadhifa zao, sina budi na mimi kujiuzulu kama walivyofanya wenzangu, kuanzia tarehe 13/6/2018,” alisema.

Ingawa wamekuwa hawataki kuweka wazi kisa cha hali hiyo, inaelezwa kwamba suala la kikosi cha Zanzibar cha vijana kupeleka wachezaji wenye umri mkubwa katika michuano ya Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ndicho chanzo kikubwa.

By Jamhuri