Klabu ya soka ya Manchester United jana imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa klabu ya Newcastle United.

Bao pekee katika mchezo huo wa ligi kuu ya soka nchini England uliomalizika jana jioni kwenye uwanja wa Saint James Park limefungwa na Matt Ritchie dakika ya 65.

 

Kwa upande wa kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameendelea kuwa na rekodi mbaya kwenye uwanja huo akiwa hajawahi kushinda mchezo wowote wa ligi.

Mourinho akiwa na Chelsea na Manchester United kwa sasa amefanikiwa kushinda mechi mbili tu kati ya tisa kwenye uwanja wa St. James Park huku mechi hizo mbili zikiwa ni za kombe la ligi (EFL CUP).

 

Matokeo ya yanaiacha Manchester United katika nafasi ya pili ikiwa na alama 56 ikiwaacha vinara manchester City wakiwa kileleni kwa alama 72.

Mechi nyingine ilikuwa ile ya Liverpool dhidi ya Southampton, ambapo katika mchezo huo liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 2-0, mabao ya liverpool yalifungwa na Roberto Firmino dakika ya 6 na la pili lilifungwa na Mohamed Salah dakika ya 42.

Liverpool wakishangilia ushindi

MSIMAMO BAADA YA MATOKEO YA MICHEZO YA JANA NA JUZI

2131 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!