Tume ya uchaguzi nchini Burundi imesema itatangaza matokeo ya kura ya maoni baadaye hii leo licha ya kiongozi wa upinzani, Agathon Rwasa kusema kuwa hatakubali matokeo hayo.

Rwasa ameitaka tume ya uchaguzi kufutilia mbali matokeo na kuitisha kura upya kwa madai kuwa kura hiyo iligubikwa na udanganyifu na vitisho kwa wafuasi wake.

Matokeo ya awali yalionyesha kuwa kura ya ‘ Ndiyo ‘ ya kuidhinisha marekebisho ya katiba imeshinda kwa kishindo.

Iwapo katiba hiyo itaidhinishwa, itamruhusu Rais Pierre Nkurunziza kuwania tena uongozi na kusalia madarakani hadi mwaka wa 2034.

1025 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!