Bondia maarufu duniani, Floyd Mayweather (36) atalipwa dola milioni 41.5 za Marekani (Sh bilioni 67.23), baada ya kumshinda Saul ‘Canelo’ Alvarez (23). Hili ni pambano la 45 kwa Mayweather akiwa ameshinda yote.

Mayweather alitarajia kuingiziwa fedha hizo kwenye akaunti yake.

 

Pambano hilo lilifanyika katika hoteli ya MGM Grande jijini Las Vegas, usiku mwishoni mwa wiki iliyopita. Katika pambano hilo la raundi 12, majaji walimpa Mayweather ushindi wa pointi na kumtangaza kuwa mshindi wa mikanda ya WBC na WBA.

 

Kila raundi moja hudumu kwa dakika tatu, hiyo ikiwa na maana ameweza kutumia dakika 36 kujipatia mabilioni hayo.

 

Alishinda kwa kupata alama 114-114, 116-112 na 117-111.

 

Hili ni pambano la pili kwa Canelo kupigwa tangu alipoanza masumbwi ya kulipwa.

1311 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!