MBUNGE wa Kishapu Mkoani Shinyanga (CCM), Suleiman Nchambi na viongozi watatu wa mgodi wa Stamigold uliyopo Tulawaka wilayani Biharamulo Kagera, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za rushwa.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Biharamulo, Hassan Mosi amesema mbunge huyo na wenzake walikamatwa na kuwekwa rumande katika gereza la wilaya hiyo Jumamosi Agosti 4, mwaka huu na leo Jumatatu Agosti 6, watafikishwa katika mahakama ya wilaya ya Biharamulo kwa kosa la kufanya miamala ya kupokea rushwa.

Mosi amesema kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha 15 cha sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kupambana na kuzuia rushwa. Aidha, ndugu, jamaa na marafiki leo wamejitokeza kwa wingi katika mahakama hiyo, huku wengi wakionekana kuwa na shauku ya kujua hatima ya viongozi hao.

By Jamhuri