Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mh John Mnyika kupitia kwenye ukurasa wake Twitter amewashukuru wakina mama wa jimbo la Kibamba kupitia kikundi chao cha VIMA kwa kumualika kushiriki shughuli ya kufunga mwaka ya kikundi hicho.

Mnyika amesema kuwa wataendelea kuwa pamoja bega kwa bega ili kuleta maendeleo ndani ya jimbo la Kibamba katika mwaka mpya 2018, hivi karibuni Mbunge huyo kupitia Mitandao ya kijamii alihusishwa kuhamia chama cha Mpinduzi, ambapo alikanusha vikali na kuwataka wana Chadema wasisikilize propoganda za mitandaoni yeye ni CHADEMA na hatakisaliti chama chake kwa gharama yoyote ile.

Wakina Mama hao piwa walimshukuru mbunge huyo kwa kuwasaidia kuwaletea maendeleo makubwa ndani ya kikundi chao na kumuomba angeze juhudi katika mpya wa 2018.

1344 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!