Mgogoro wa Israel na Palestina -6

Wiki iliyopita tulishuhudia Serikali ya Uingereza ikishindwa kutekeleza ahadi zake ilizozitoa juu ya Palestina kuwa taifa. Wiki hii unaletewa sehemu ya sita ya makala hii inayosimulia mgogoro wa Israel na Palestina. Endelea…

 

Baada ya Serikali ya Uingereza kuwa imeelemea upande mmoja; dhamira na malengo ya Wazayuni yalikuwa  ni kuhakikisha utekelezaji wa Azimio lile (The Balfour Declaration) kwa msaada wa wakubwa hawa  – Waingereza, na kwa ujumla  – walifanikisha. Udhamini  ambao ulikuwa umesimamiwa na League of Nations kwa niaba ya Great Britain mnamo mwaka 1922 kuitawala Palestina ulibainisha kwamba Mandatory ingekuwa na wajibu wa kutekeleza Azimio lile mnamo 2 November 1917- kwa dhamira ya kuanzishwa kwa  Taifa  la Wayahudi ndani ya Palestina ( establishment in Palestin a national home for the “ Jewish People”.

Itakumbukwa kwamba Bunge la Mabwanyenye na Uingereza ( English House of Lords) lilipinga kuunganishwa kwa Azimio la Balfour katika udhamin wa Palestina. Katika mjadala wa Bunge hilo, June 21, 1922 wazo hili halikukubalika. 

Lord Islington alisema – “Linavunja  moja kwa moja ahadi zilizotolewa  na Serikali ya Kifalme kwa watu wa Palestina. Zaidi ya hapo vifungu vinavyohusu uanzishwaji  wa Taifa la Wayahudi vilikuwa vikipingana na kifungu namba 22 cha makubaliano ya League of Nations ambacho kiliweka msingi wa kanuni kuu ya mfumo wa udhamini.”

Azimio hili linaishinikiza Uingereza kwa kuitwika jukumu la udhamini kwa kufanya Wazayuni kuwa na nguvu za kisiasa wakati 90% ya wakazi si Wayahudi. Kusema ukweli Waothodox wengi ni Wayahudi si Palestina, na iko hivyo duniani kote kwa ujumla.

Wapalestina wanaliangalia suala hili katika mtazamo hasi. Hawapendi kanuni kuu (principle) hii ya- zionist home in Palestine.

Mradi huu wa Wazayuni una dhamira ya kuwafanya wawe wenyenguvu za kisiasa nchini Palestina kwa kuwarejesha Wayahudi wengine wakimbizi kutoka sehemu nyingine duniani. Mradi huu wa kuwarejesha wayahudi wakimbizi katikati ya nchi yenye tabaka la wakazi  wenyeji ni sawa na hekaya za  abunuwasi katika zama hizi. Ni uzoefu usiokuwa wa asili – ni kinyume cha kanuni ya asili.

Kwa mantiki hii maridadi, ni mradi unaozua balaa na janga kubwa “ ( This scheme of importing an alien race into the midst of a native local race is flying in the every face of the  whole  tendencies of the age. – It’s an unnatural experiment – It’s  literally inviting subsequant catastrophe”)

Akijibu mapigo ya kauli ile, Arthur wa azimio lile- Lord Balfour alisema, Uzayuni unaweza kushindwa hili ni tukio kwani   “tumeshakoma kuwa  watu wa matukio? Hatuwezi kujaribu  majaribiio mengine?” Lord Sydenham alimjibu mwandishi wa azimio hili akisema  “Jaribio la Uzayuni lingeshindwa”.

Lakini machungu yanayosababishwa na kurundikwa kwa wakimbizi wa kuja kwenye nchi ya kiarabu/ waarabu wote duniani – hawawezi kuhakikiwa. “Tulichokifanya, kimsingi si kwa minajiri ya Wayahudi- bali ni kusaidia kutunisha misuri na ubabe wa sera za Kizayuni. Matokeo yake ni kuanza kuuguza kidonda ndugu katika ukanda wa Mashariki ya Mbali na hakuna anayeweza kusimama kifua mbele na kutuhakikishia kidonda kile kitapona baada ya muda gani”. Maneno haya ya kinabii bado yanatamalaki katika ukweli hadi leo.

Mjadala ule ulipigiwa kura na matokeo yake yakawa kura 60 vs 29. Hii ilimaanisha utekelezwaji wa Azimio la Balfour, lakini katika mjadala wa Bunge la Makabwela la Uingereza (The House of Commons). Hoja iliyotaka kwamba mamlaka kwa ajili ya Palestina ingepaswa kuthibitishwa na Bunge ilipigwa mweleka. Kuhusishwa kwa hoja hii kuliiwezesha Serikali ya Uingereza, wiki tatu baadaye kuthibitishwa kwa mwangalizi wa Palestina na Council  ya League of Nations. Kwahiyo suala hilo halikupitishwa na Bunge la Makabwela, wala la Mbwanyenye.

Na hapa tujiulize sasa. Ilikuwa na maana gani – maelezo yasemayo, “National home in the Balfour Declaration”? – Yaani Taifa la Israel ndani ya Azimio la Balfour.

Ni maelezo kanganifu – na kwa ujumla wake haileti maana inayokubalika. Hata hivyo, licha ya ukanganifu wake – si upande wa Azimio la Balfour- lililojulikana kama Wayahudi wa Kizayuni, wala Serikali ya Uingenreza – iliyodhamiria kukabidhi haki za ki- mipaka  ( territorial rights) kwa Wayahudi au yalichangia kutwaliwa kwa uhuru wa kujiamulia mambo kwa Palestina.

 

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa Anapatikana kwa:-

 (+255)784  142  137

(+255) 713 333141

Au  barua  pepe

[email protected]

[email protected]