Mgogoro wa Israel na Palestina -7

Wiki iliyopita katika sehemu ya sita tulishuhudia mchango wa Uingereza katika mgogoro wa Israel na Palestina. Leo, tunakuletea sehemu ya saba ya makala hii inayosimulia mgogoro huo. Endelea…

 

Norman Benwitch, Muyahudi-Mzayuni ambaye alishika wadhifa kwa muda mrefu katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu Palestina wakati wa usimamizi wa Uingereza, aliwahi kutamka mara kadhaa kwamba  [Israel] uhuru wa kujiamulia mambo yake yenyewe (sovereignty) haikuwa sehemu ya nchi ya ahadi ya Wayahudi.

Alisema; state sovereignty si  muhimu kwa national ideal. Uhuru kwa Uyahudi kujiendeleza kwa manufaa yake ya kiutamaduni katika mazingira yake ndiyo jambo mahususi na si madai ya ujumla wake.

Aliandika pia;

“Kumekuwa na zuio kwa matumaini ya Wazayuni ya kwamba Waarabu Waislamu kwa sasa ambapo wanamiliki ardhi ya Palestina – wakiwa tayari wanazidi robo ya milioni – hawawezi kufurushwa. Lakini haitegemewi wala kutumainiwa ya kwamba Wayahudi wanapaswa kuhodhi na kutumia ardhi yote ya Palestina.”

Benwitch alielezea dhana ya nchi ya ahadi ya Wayahudi haileti mantiki ya unyakuaji wa haki zote za uamuzi wa kisiasa bali ni wasaa tu kwa ajili ya  maendeleo ya kitamaduni.

Vivyo hivyo, mwandishi wa Kiingereza wa Azimio la Balfour, hakumaanisha wala kudhamiria ukabidhishaji wa haki ya uamuzi wa kisiasa kwa Wayahudi ndani ya Palestina. Katika maelezo yake ya sera mnamo 1922 serikali ya Uingereza ilitamka kwamba tafsiri ambayo kwayo serikali ya kifalme iliainisha Azimio la 1917 si kwa minajili ya kutibua wakazi wengi wa Kiarabu katika ardhi ya Palestina. 

Mnamo mwaka 1922, Winston Churchill alizungumza yafuatayo katika Bunge la Makabwela (The House of Commons): 

“Kwa wakati mmoja, ahadi hii ilitolewa kwa Wazayuni. Ahadi hiyo muhimu ilitolewa kwa wakazi Waarabu wa Palestina kwamba haki zao za uraia na zile za kidini (imani) zingelindwa kikamilifu na kwamba zisigeuzwe na kutoa nafasi/mwanya kwa wageni.

Hebert Samwel ambaye binafsi alikuwa Mzayuni mkereketwa na wa kwanza kunadi sera hizi mbele ya Baraza la Mawaziri la Uingereza, alitafsiri Azimio la Balfour kuwa halihusishi uundwaji wa dola ya Kiyahudi, kwa kusema; “Dola ya Kiyahudi imekuwa ni dhamira ya Wayahudi kwa karne nyingi. Ni dhamira ambayo kwa kipindi hiki haiwezi kuthibitika. Haijumuishwi katika Azimio la Balfour. Hapakuwa na ahadi ya dola ya Kiyahudi kilichoahidiwa ni kwamba Serikali ya Uingereza ingependelea kuundwa kwa nchi ya ahadi ya Wayahudi – msamiati ulichaguliwa kwa umakini Palestina.”

Azimio halikusema Palestina itakuwa Taifa la Wayahudi ndani ya Palestina, bila kugusa haki za kiraia na zile za kidini za wakazi wa Kiarabu.

Kama mtu mwenye akili timamu atakubaliana na tafsiri zote hizi (nilizozieleza) inaonekana kwamba dhamira ya Azimio la Balfour haikuwa kuundwa kwa dola ya Kiyahudi bali ni kuanzishwa kwa kitu tofauti.

Zaidi ya yote, bila kujali ukweli wa tafsiri ile, Azimio la Balfour linakinzana na uhakikisho wa ahadi kedekede zilizotolewa na Serikali ya Uingereza kwa Waarabu katika ujumla wake na kwa Wapalestina kwa umuhimu wake. 

Hakikisho hizi na ahadi zilijumuishwa katika mawasiliano ya MC Mahon Hussein ya 1915-1918- Ujumbe wa Hogarth wa Januari 1918.

Matamko ya Juni 7, 1916, Anglo-French Declaration la November 1918- na Uhakikisho wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa wakazi wa Palestina, Syria na Lebanon yana nafasi.

Katika mkutano wa Anglo-Arab kule London mwaka 1939, kamati ilijizatiti kuzingatia mawasiliano ya MC Mahon Hussein  (1915-1916) – na kufikia hitimisho ya kwamba kauli zilizotolewa kabla na baada ya vita kwamba Serikali ya Kifalme haikuwa huru kuingilia Palestina dhidi ya matakwa ya Wapalestina na kwamba statement zote hizi zinapswa kuzingatiwa. 

 

>>ITAENDELEA.

 

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa Anapatikana kwa:-

 (+255)784  142  137

(+255) 713 333141

Au  barua  pepe

[email protected]

[email protected]