Aliyekuwa mwakilishi wa Kenya katika mashindano ya Big Brother Afrika mwaka huu, Huddah Monroe, amekanusha tuhuma dhidi yake kwamba ana Virusi vya Ukimwi kutokana na mwili wake kupungua kupita kiasi.

Mrembo huyo ambaye tayari ametolewa katika mashindano hayo amekanusha tuhuma hizo katika mahojiano na Kituo cha Radio cha Gheto nchini Kenya, hivi karibuni.

 

Amebainisha kuwa kilichomsababisha akonde ni dawa za kulevya aina ya cocaine, bangi na nyingine zenye nguvu kubwa mwilini na hivyo kusababisha kupungua ghafla.

 

Mrembo huyo amesema kwamba aliamua kutumia dawa za kulevya kupunguza msongo wa mawazo, lakini akasema kwamba kwa sasa ameachana na matumizi ya dawa hizo kurejesha afya yake.

 

Hivi karibuni, Huddah alifunguka kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba hivi sasa hatumii aina yoyote ya dawa za kulevya wala kilevi cha aina yoyote.

 

1232 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!