Mtulia (Katikati) aliyeshika kadi ya Chama Cha Mapinduzi Akiapa wakati wa kukabidhiwa kadi hiyo.

 

ALIYEKUWA Mbunge wa Kinondoni kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia amekabidhiwa rasmi kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mapema leo katika ofisi za chama hicho.

 

YALIYOSEMWA NA ALIYEKUWA MBUNGE WA KINONDONI KUPITIA CUF MAULID MTULIA MARA BAADA YA KUKABIDHIWA KADI YA CCM LEO JUMATATU TAREHE 04/12/2017

 

“Nimejivua nyadhifa zangu zote ya Ubunge wa Kinondoni na vyeo vyote nilivyokuwa navyo CUF na kuamua kujiunga na CCM kutokana na kuridhishwa na CCM ya sasa na utendaji wa Rais Dk. Magufuli.

 

“Mimi ni mgeni na salamu ninayoijua ya CCM ni CCM Oyeee. Nimejiunga na CCM ili kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais Dk. Magufuli. Nimetoka kwenye chama chenye migogoro mingi, nimekuja kwenye chama chenye amani, haki na Demokrasia ya kweli. Ningekuwa Mbunge kupitia CCM ningefanya mengi makubwa zaidi,” alisema Mtulia.

 

2044 Total Views 4 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!