MultiChoice Africa imezindua rasmi kituo cha mafunzo ya uandaaji wa filamu  katika ukanda wa Afrika Mashariki . Sherehe za uzinduzi huo zimefanyika mjini Nairobi nchini Kenya katika makao makuu ya ofisi ya MultiChoice na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu pamoja na wawakilishi mbalimbali wa serikali  kutoka katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.

Baadhi ya viongozi wa serikali waliohudhuria katika uzinduzi huo mjinji Nairobi ni pamoja na Waziri wa Habari, Teknolojia na Mawasiliano Kenya, Mhe. Joe Mucheru, Katibu wa Wizara ya Habari na Mawasilano Kenya, Bi Fatma Hirsi, Mwenyekiti wa Baraza la Filamu nchini Kenya Chris Foot, Mwenyekiti wa bodi ya Filamu nchini Kenya Ezekiel Mutua, Kaimu Mkurugenzi Mkuu KBC Paul Jilani, wajumbe wa kamati ya bunge ya ICT kutoka Kenya akiwemo mheshimiwa John Kiarie huku Tanzania ikiwakilishwa kwa heshima kubwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza.

 

By Jamhuri