Bingwa wa Wimbledon katika mchezo wa tenisi, Andy Murray ameshindwa katika mashindano ya mchezo huo  baada ya kufungwa mpinzani wake Ernests Gulbis katika raundi ya tatu ya kombe la Rogers Cup mjini Montreal.

Gulbis raia wa Latvia ambaye kwa sasa anashika nafasi ya 38 katika orodha ya wachezaji bora wa tenisi duniani,alishinda kwa seti mbili katika ushindi mfulululizo wa matokeo ya 6-4 6-3.

 

Mashindano hayo ya Montreal yenye ushindani wa kila aina kutokana na wachezaji kukamiana ni ya kwanza kwa Murray tangu ashinde ubingwa wa Wimbledon mwezi uliopita.

 

Hata hivyo baada ya kukosa ushindi, Murray alisema hana wasiwasi bali anajiona kama mchezaji mwenye kibarua cha kujifua zaidi kabla ya kushiriki katika kabla ya mashindano mengine ya ubingwa wa tenisi ya Marekani.

 

Murray, ameshawahi kushinda mara mbili nchini Canada lakini safari hii Gulbis alimkatiza katika safari yake ya kunyakua ubingwa, Hii ni mara ya kwanza kwa Gubis kumshinda Murray katika mechi sita walizokutana.

 

Awali wapinzani wakubwa wa Murray,Rafael Nadal na Novak Djokovic walionyesha viwango vya hali ya juu baada ya kushinda mapambano yao. Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 24 Canada imewakilishwa katika robo fainali na wachezaji wawili Vasek Pospisi na Milos Raonic.

 

By Jamhuri