Mtu aliyetuhumiwa kwa kuuza nyama ya paka wauzaji sambusa amehukumwa kifungo cha miaka mitatu na mahakama ya Nakuru

Hakimu mkuu Benard Mararo alimhukumu James Mukangu Kimani baada ya kukiri kosa hilo alipowasili katika mahakama hiyo siku ya Jumatatu.

Bwana Kimani alishtakiwa kwa kuchinja na kuuza nyama ya paka kwa wateja wake mnamo mwezi Juni 24 mjini Nakuru.

Alishtakiwa kwamba alimchinja paka kwa matumizi ya binaadamu kinyume na sheria ya chakula , dawa na kemikali.

Mwanamume huyo alikamatwa Jumapili ambapo inadaiwa alipatikana akimchuna ngozi paka.

Gazeti la Star linasema mwenyewe alikiri kupika sambusa akitumia nyama hiyo.

Taarifa kwenye vyombo vya habari Kenya zinasema mwanamume huyo alikiri kuuza nyama ya paka zaidi ya elfu moja mjini humo tangu mwaka 2012.

 

1637 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!