Kwa uzito wa busara kubwa iliyotumika katika salamu hizo za rambi rambi na kwa kuogopa kupotosha uzito huo nalazimika kuziwasilisha kwa lugha hiyo hiyo ya kiingereza kama ifuatavyo;
“For the men and women who have served the great cause of development in the world, one of the lights of our lives went out today. Mr. Julius Nyerere was one of the founding fathers of modern Africa. He was also one of the few world leaders whose high ideals, moral integrity, and personal modesty inspired people right around the globe.


While  world  economists  were  debating  the  importance  of  capital  output  ratios, President Nyerere was saying that nothing was more important for people than being able to read and write and have access to clean water.
He gave his compatriots a sense of hope and achievement early in their life as a country. And he gave them a sense of nation while few parallels in Africa and the world-bound by a common language (Kiswahili) and a history almost entirely free of internal divisions and conflict. His political ideals, his deep religious convictions, his equally deep religious tolerance, and his belief that people of all ethnic and regional origins should have equal access to knowledge and material opportunities have marked his country –and Africa -forever.


He was a leader in the liberation of Southern Africa. He looked after hundreds of thousands of refugees forced to live in western Tanzania by political turmoil in central Africa. And he left office peacefully at an age when he could certainly have continued. He was known as “Mwalimu”(or “Teacher”) –which was his –first profession. Many of us still regard ourselves as his students, and we feel very honored to have known and worked with in his life.
To people of Tanzania –and to his wider family across. Africa and around the world –I want to say how much we share your sadness at his passing. However, the example he sent and the ideals he represented will remain a source of inspiration and confort for all of us. That is a legacy which even President Nyerere –modest as he was –would have been proud of.


Huyo ndiye Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tunayemjadili na hiyo ndiyo thamani ya Baba wa Taifa alivyoonekana kimataifa. Dhahili mawazo ya Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere yataendelea kuwa na thamani zaidi ya karne tatu zijazo alikuwa ni mali ya Tanzania, Mali ya Afrika na mali ya Dunia. Kuna nyakati baadhi ya kauli zake ziliheshimika kuwa Tanzania imezungumza au Afrika imezungumza au Dunia imezungumza. Mwalimu alikuwa na maono ya taifa lake (clear vision) alijua ni wapi taifa lake linaelekea.
Hivyo aliposema kwa jeshi jipya la watanzania kwamba nendeni mkaipende Tanzania kama mama zenu kwake yeye ilikuwa ni programu ya kudumu katika ustawi wa taifa la Tanzania kijamii, kisiasa na kiuchumi. Ingawa alikuwa yuko tayari kwenda na mazingira lakini alikuwa na msimamo wa dhabiti wa kutoyumbishwa katika Uzalendo, Uadilifu na Utaifa.

3.9:   Nyerere na Rushwa  .
Katika eneo hili kabla sijasema chochote kuhusu Nyerere na rushwa naomba nianze kwa kusema kwamba – Ripoti ya Tume ya Jaji Warioba ya mwaka 1996 ndiyo kipimo cha hali yetu kitaifa kuhusu ombwe kubwa la Uadilifu ambapo rushwa imeendelea kuwa ni tatizo kubwa katika nchi yetu.
Pamoja na ripoti hiyo kuendelea   kuwekwa hadharani siku hizi na Gazeti la Jamuhuri – ningeshauri yale yaliyomo katika ripoti hiyo iwapo kweli uadilifu ni swala tunalo lithamini katika maendeleo ya nchi yetu Tanzania basi ni muhimu taarifa hiyo ya Warioba ikapewa uzito stahiki kwa kufanyiwa kazi na serikali.
Tukirudi nyuma kabla ya uhuru tunaona katika hansard ya kikao cha 35 tarehe 17 Mei, 1960, upo ushahidi mkubwa tu wenye kuonyesha Uzalendo, Uadilifu na Utaifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere anakemea vikari rushwa. Akiwa bungeni katika mjadala wa bajeti pamoja na mambo mengine Mwalimu akichangia alisema; nanukuu;


Sasa Mhe. Nitakuwa mnafiki nikisema mambo yako sawa kwa sasa wakati ni ukweli kwamba hali ni kinyume. Ipo rushwa kwa hiyo Mhe.naamini kuwa lazima rushwa ishughulikiwe bila huruma kwa sababu ninaamini kuwa rushwa nahongo ni madui wakubwa zaidi kwa ustawi wa wananchi kuliko VITA! Binafsi ninaamini rushwa ndani ya nchi, lazima ishughulikiwe kama UHAINI. Iwapo watu hawana imani na serikali yao, iwapo watu wanaamini kuwa HAKI INANUNULIWA, watu wa aina hiyo watabaki na matumaini gani?
Kwa watu wa aina hiyo suluhisho ni kushika silaha na kuiondoa madarakani serikali hiyo ya kipuuzi. Maana hawatakuwa na matumaini tena juu ya maendeleo yao.
Mhe. naamini kuwa tutakapo anza kwenda mbele, ili tuweze kupigana vizuri juu ya umaskini, maradhi na ujinga HATUNA BUDI KUAMINIWA NA WANANCHI.


Shuruti tuwe na watumishi ndani ya serikali za mitaa,vyama vya wafanyakazi, vyama vya ushirika, ndani ya utumishi wa umma na serikali kuu yenyewe,ambamo wanachi wana imani nao pasi na shaka. Mwalimu Nyerere aliendelea kujadili juu ya nafasi ya mwafrika na juu ya mishahara na akapendekeza kupunguzwa kwa mishahara ya Mawaziri wa kuchaguliwa. Hilo lilitekelezwa baada ya TANU kushinda uchaguzi na Mwalimu Nyerere kuwa Waziri Mkuu. Kadharika baada ya kuwa Rais Mwalimu alishusha mshahara wake kwa asilimia ishirini.
Ndugu zangu katika nukuu hii iliyosheheni busara za Uzalendo, Uadilifu na Utaifa ambapo Mwalimu alisema rushwa ni sawa na kansa na ni mbaya kuliko vita, sasa mimi niongeze  nini zaidi! Hali ikoje katika serikali za mitaa, wizara na idara za serikali na taasisi za umma. Je kazi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali inachukuliwa kwa uzito gani katika taifa letu. Yote nayaacha kwenu kwa tafakuri za kina kwamba hali ikoje sasa katika taifa letu! Naomba nichomekeze hapa ambayo nilishawahi kuyasoma katika mtandao. Kwamba familia moja ilikuwa na wasomi wazuri sana wanne mmoja na PHD ya Uchumi, mmoja ni Daktari wa Binadamu na mwingine ni Mhandisi wa Maji wote hawa watatu hawakuwa na ajira. Mtoto wa nne pamoja na kuwa na kisomo kizuri kama Mhasibu mkuu wa Idara fulani  huyu  alikuwa  ni  mwizi  aliyekubuhu  majirani  na  jirani  waliomzunguka walijua hivyo!
Kufuatia heshima kubwa ya familia ya watoto hao majirani walikwenda kupeleka ushauri kwa wazazi hao kuwa huyo mtoto mwizi anaharibu heshima ya familia hiyo na kwamba wazazi hao washirikiane na majirani kumstaki kwa mtoto huyo mwizi kwa ushahidi mkubwa waliokuwa nao! Jibu la mwaka lililotolewa la wazazi wa mtoto mwizi lilikuwa kuwa mbona mtoto huyo ndiye tegemeo la ustawi wa maisha ya wazazi hao kwa nini ashitakiwe. Haiwezekani. Shauri yenu nyie mlio na watoto wasiojua kutumia kalamu vizuri. Kwa umaskini wenu mtajijua na Mungu wenu! Je malezi haya ya mwizi kutukuzwa ndani ya jamii yetu hapa Tanzania hayapo? Tafakari!


3.10: Nyerere na Uzalendo, Uadilifu na Utaifa Katika Kuheshimu Katiba ya Nchi.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni mtiifu mkubwa wa katiba ya serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Aliheshimu sana utawala wa sheria na mwenye kutetea haki na usawa wa binadamu na jasiri katika kusimamia na kutetea masuala ya msingi. Katika hili alikuwa ni mwepesi wa kukemea/kuonya na kushauri kwa ujasiri usio kifani kwa mfano suala la kasoro mbalimbali katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

3.11: Uzalendo, Uadilifu na Utaifa wa Nyerere katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika.
Katika hulka ya daima ya kufikiria watu (raia) katika kukuza ustawi wa maendeleo yao (People centrered – development attitude) – Mwalimu Nyerere akiendelea kuchangia bungeni tarehe 17 Mei, 1960 alisema nanukuu;
“Mhe. Si rahisi kujua hatima ya Kamisheni ya Afrika Mashariki ningependa kujizuia kufafanua juu ya suala hili kwa sababu zilizo bayana. Mhe. Jambo la maana ambalo lingestahili kufanyika ni kushughulikia nchi hizi kuwa kitu kimoja kiuchumi na kisiasa. Tunajaribu kujenga nchi hizi si kwa minajiri ya ufahari bali kama vyombo vya kuwapatia watu wetu bidhaa zinatokanazo na uhuru. Naamini jinsi nchi hizi zinavyozidi kuwa kitu kimoja kikubwa, ndivyo zinajiongezea uwezo wa kuwahudumia vizuri watu wake na kujiamini zaidi katika kupigana vita dhidi ya umaskini, maradhi na ujinga. Kwa hiyo hatua ya kuzileta pamoja nchi hizi sharti ziungwe mkono. Nasi katika Tanganyika hatuwezi kukatisha tamaa juhudi hizo!

INAENDELEA>>

1839 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!