NAIBU Spika wa Bunge, Dkt.  Tulia Ackson amemwapisha Mmwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dkt. Adelardus Kilangi bungeni na kumkabidhia vitendea kazi kabla ya kuanza kwa Kikao cha Tano cha Mkutano wa 11 wa Bunge, Mjini Dodoma, leo Feb 5, 2018.
Dkt. Kilangi ambaye amekula kiapo cha uaminifu, aliteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Mgufuli,  Februari Mosi, 2018 na Paul Ngwembe aliteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Katika hatua nyingine,Magufuli alimtea aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na naibu wake, Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambao waliapishwa juzi Jumamosi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
3104 Total Views 12 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!