Mhariri,

Nimekuwa nikifuatilia haki yangu katika mahakama kwa miaka 14 sasa bila mafanikio. Kwamba nimekuwa nikifanya jitihada za kuomba kukutana na Mheshimiwa Jaji Mkuu, lakini hadi sasa sijafanikiwa kutokana na kunyimwa nafasi hiyo na watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Ninahitaji kukutana na Jaji Mkuu, Mohammed Chande Othman nimweleze shida yangu kwamba nina wasiwasi kuwa uamuzi usiyo wa haki ulifanyika na kupindisha sheria katika malalamiko yangu, hivyo kuecheleweshwa haki yangu.

Mpaka sasa nina viambatanisho (vielelezo) vyote vinavyothibitisha ninachokilalamikia.

Tafadhali sana, kupitia barua hii, ninaomba mamlaka husika zinisaidie niweze kupata haki ya kukutana na Mheshimiwa Jaji Mkuu ili nimweleze kero yangu anisaidie kwa kujibu wa sheria.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu. Mungu awabariki. Asanteni.

Edward Msago,

Dar es Salaam.

1115 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!