Nyerere: Uanachama CCM ni hiari

“Uanachama wa CCM ni wa hiari. Kuwa na kadi ya CCM si sharti la kupata kazi, au huduma ya umma, au leseni ya biashara, au haki yoyote ya raia wa Tanzania.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Dilma: Ndiyo, wanawake wanaweza

“Natumaini baba na mama wa wasichana wadogo watawaangalia na kusema ‘ndiyo, wanawake wanaweza’.”

Hii ni kauli ya Rais Dilma Rousseff wa Brazil, ambaye ni mwanamke wa kwanza kukabidhiwa wadhifa huo nchini humo.

 

Pengo: Tujenge amani Tanzania

“Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika taifa letu… amani ya taifa letu ni jambo la msingi.”

Haya ni maneno ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycap Kadinali Pengo.

 

Hollande: Uchaguzi unahitaji ujasiri

“Katika uchaguzi, mtu anahitaji kuwa na matumaini pamoja na ujasiri.”

Haya yalisemwa na Rais wa 24 na wa sasa wa Ufaransa, Francois Hollande.

1282 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!