Nyerere: Jeshi letu ni la Kizalendo

“Jeshi letu haliwezi kuwa Jeshi la mamluki, ni Jeshi la Kizalendo. Matumaini yangu ni kwamba Jeshi letu litaendelea kulinda na kutetea misingi mikuu ya Azimio la Arusha.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye pia ni mwasisi wa Azimio la Arusha.

Napolitano: Shule za Serikali ni za wote

“Shule za Serikali ziliundwa kwa ulinganifu mkubwa wa jamii yetu – mahali ambapo watoto wote wanaweza kupata fursa za kielimu kujiandalia maisha ya ukubwani.”

Haya ni maneno ya Janet Napolitano, Katibu wa Usalama wa Ndani wa Marekani. Ndiye mwanamke wa kwanza kupata wadhifa huo nchini humo.

 

Lowassa: Sekondari za kata ni mkombozi

“Shule za sekondari za kata ni kielelezo cha usawa wa elimu kwa Watanzania, ni mkombozi wa mtoto wa mwananchi kule kijijini.”

Kauli hii ilitolewa na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Monduli.

 

Shinawatra: Wathailand ni wastahimilifu

“Ninaamini watu wa Thailand ni wastahimilifu, na watu ambao angalau wananipa nafasi ya kuthibitisha uwezo wangu wa kuwasaidia.”

Hii ni kauli ya Waziri Mkuu wa 28 wa Thailand, Yingluck Shinawatra, ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu nchini humo.

By Jamhuri