Julius nyerere: Usipowapa wengi watanyakua

“Utaratibu wowote unaowanyima wengi haki yao hauwezi ukaitwa demokrasia… Waswahili wanasema: Wengi wape, usipowapa watanyakua wenyewe.”

Haya ni maneno ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, wakati akihimiza demokrasia ya kweli.

Ellen Sirleaf: Elimu inaboresha maisha

“Kama wanaume wengi wamesoma zaidi na wanawake wameelimika, mfumo wa thamani unatakiwa kuboreshwa zaidi… na maisha ya binadamu yawe mazuri zaidi.”

Kauli hii ni ya Rais wa 24 na wa sasa wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf. Alipata kuwa Waziri wa Fedha wa nchi hiyo chini ya Rais William Tolbert, mwaka 1979 – 1980.

 

Joseph Blatter: Mpira wa miguu unaweza kuona

“Ni muhimu sana kuona kwamba mpira wa miguu unaweza kuona zaidi ya dini lakini FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa) haiwezi kupuuza madhara yake.”

Maneno haya ni ya Rais wa nane na wa sasa wa FIFA, Joseph ‘Sepp’ Blatter, ambaye pia ni kiongozi wa soka nchini Uswissi.

 

Mary Mwanjelwa: Tuwatafutie vijana ajira

“Tunalo tatizo la soko la ajira, hali hii inawafanya vijana wengi warande barabarani na mwisho wa siku hujikuta wakitumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa wenye maslahi yao binafsi na siyo ya Watanzania.”

Haya yalinenwa na Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania, Dk. Mary Mwanjelwa.

1388 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!