Mwalimu Nyerere: Tukatae mawazo ya kipumbavu

“Watu tunaafikiana na wazo, lakini mawazo ambayo waziwazi ni ya kijinga lazima tuyakatae. Mtu mwenye akili timamu akikupa mawazo ya kipumbavu, usipoyakataa anakudharau. Sasa hatuwezi kukubali mambo ya kipumbavu Tanzania.”

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, aliyasema haya kuhimiza watu kuwa makini katika kupokea mawazo ya wengine.

Paul Sozigwa: Siwezi kuhonga, ninaweza kulima

“Niligombea ujumbe wa NEC (Halmashauri Kuu ya Taifa) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), nikashindwa kwa sababu sikuhonga. Nilikataa kuhonga na hadi leo sitaki. Mimi siwezi kuhonga ili kutafuta cheo, nina uwezo wa kulima.”

Kauli hii ni ya kiongozi wa zamani wa Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Sozigwa.

 

 

Salma Kikwete: Tuzuie maambukizi mapya Tanzania

“Siku zijazo za nchi yetu zinategemea afya ya kizazi chake kijacho, lazima tufanye kila tuwezalo kuhakikisha hakuna maambukizi mapya kwa vijana wa Tanzania.”

Maneno haya ni ya Mke wa Rais, Salma Kikwete, wakati akizindua Mpango wa Bima ya Afya kwa vikundi vya wajasiriamali nchini, Septemba 26, 2012.

 

Steve Jerald: Tofauti ya kusoma na kuelimika

“Ipo tofauti ya kusoma na kuelimika. Waliosoma na kuelimika hutumia maarifa waliyoyapata kwa manufaa ya jamii. Wanapoyatumia maarifa yao kwa manufaa yao binafsi, ni ushahidi kwamba walisoma bila kuelimika.”

Haya yalinenwa na mwanafalsafa wa nchini Marekani, Steve Jerald, wakati akifafanua tofauti ya kusoma na kuelimika.

 

 

 

By Jamhuri