Julius Nyerere: Tusiruhusu wachache kuishi kifahari

“Kama watu wachache wanaishi maisha ya fahari fahari, na watu walio wengi hawapati hata mahitaji yao ya lazima, hatutaweza kudumisha amani na utulivu nchini mwetu. Ni muhimu sana kwa chama chetu na serikali yake kulizingatia jambo hili kwa makini.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mother Teresa: Upendo huanzia nyumbani

“Upendo huanzia nyumbani, na sio kwa kiwango kipi tunaufanya… bali kwa kiwango gani tunauweka upendo huo katika vitendo.”

Haya ni maneno ya mtawa (sista) wa Kanisa Katoliki wa nchini India, Mtakatifu Teresa wa Calcutta anayejulikana zaidi kwa jina la Mother Teresa.

 

Robert Frost: Fanyeni kazi kwa uaminifu

“Kwa kufanya kazi kwa uaminifu kwa saa nane kwa siku, hatimaye unaweza kupata kuwa bosi na kufanya kazi kwa saa kumi na mbili kwa siku.”

Kauli hii ni ya mtunzi wa mashairi maarufu wa nchini Marekani, Robert Lee Frost. Mashairi yake yalianza kuchapishwa Uingereza kabla ya kuchapishwa Marekani.

 

Park Geun-hye: Nitakomesha mgawanyiko, migogoro

“Nitakomesha historia ya mgawanyiko na migogoro kwa njia ya maridhiano na haki.”

Hii ni kauli ya Rais wa 11 na wa sasa wa Korea Kusini, Park Geun-hye. Ndiye mwanamke wa kwanza kupata wadhifa huo nchini humo.

By Jamhuri