NUKUU ZA WIKI

Nyerere: Nilipata ajali ya kihistoria

“Kitaaluma mimi ni mwalimu wa kufundisha darasani; lakini kwa sababu ya ajali ya kihistoria nilijikuta nikiwa kiongozi wa mapambano ya kudai uhuru na baadaye kiongozi wa nchi yetu.”

 

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Theresa: Kutotakiwa ni umaskini mkubwa

“Kuwa mtu asiyetakiwa, asiyependwa na asiyeheshimiwa, kwa mtazamo wangu, hiyo ni njaa kubwa kushinda njaa yoyote, na ni umaskini mkubwa kushinda hata ule wa mtu asiye na chakula.”

 

Haya yalisemwa na Mtawa wa Kanisa Katoliki nchini India, Mother Theresa ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel.

 

Sokoine: Wanaoharibu mazingira wabanwe

“Miti na misitu inaungua kila mara. Wanaounguza utajiri huu wanaachwa na wengine wanafanya hivyo kwa ukorofi. Hatuwezi kuchezea maisha yetu wenyewe. Lazima sheria iwabane wote wanaohusika kuharibu mazingira.”

 

Kauli hii ilitolewa na Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine.

 

Gandhi: Si rahisi mtu mnyonge kusamehe

“Si rahisi kwa mtu mnyonge kusamehe. Kusamehe ni sifa ya wenye nguvu.”

 

Haya ni maneno ya Baba wa Taifa la India, Mohandas Karamchand Gandhi, maafuru kwa jina la Mahatma Gandhi.