Bill Getes: Kukumbuka ulipokosea ni muhimu

Ni vizuri  kusherehekea mafanikio lakini ni muhimu zaidi kukumbuka uliposhindwa awali.

Kauli hiyo ilitolewa na mfanyabiashara mkubwa  wa Marekani na Mwenyekiti wa Microsoft. Bill Gates.

Albert Einstein: Maarifa ni muhimu

Mawazo ni muhimu zaidi kuliko maarifa.

Kauli hiyo ilitolewa na mwanafizikia kutoka Ujerumani Albert Einstein

 

Michael Jackson: Sitaacha kuwapenda watu

Sitaacha kamwe kuwapenda watu na kuwasaidia kwa njia ya Yesu.

Kauli hii ilitolewa na Mwanamuziki na Mfalme wa Pop duniani Michael Jackson

 

Nyerere: Hakuna watu kwa watu wengine

Hakuna Taifa lenye haki ya kufanya maamuzi kwa ajili ya Taifa lingine na hakuna watu kwa watu wengine.

Kauli hii ilitolewa na Rais wa Kwanza wa Tanzania Marehemu Julius Nyerere  Januari 1, 1968, alipotoa Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya.

3036 Total Views 3 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!