Nyerere: Viongozi wabovu hulizwa na matatizo

“Viongozi wabovu wenye mioyo ya kuku, hulizwa na matatizo; bali watu madhubuti, wenye mioyo thabiti, hukomazwa nayo… hatima ya nchi yetu ni jukumu letu. Kwa pamoja tunaweza kuisaidia nchi yetu kusonga mbele kuelekea kwenye haki zaidi na usawa zaidi kwa Watanzania wote.”


Haya ni maneno ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Helen Keller: Bora kutembea na rafiki gizani

“Kutembea na rafiki gizani ni vizuri zaidi kuliko kutembea mwenyewe kwenye mwanga.”


Maneno haya ni ya mwandishi na mhadhiri wa nchini Marekani, Helen Keller.

 

Jaji Samatta: Mafisadi wako hadi ngazi ya kijiji

“Mafisadi inasemekana sasa wako hadi ngazi ya serikali za vijiji. Nisomapo baadhi ya makala magazetini na kusikiliza baadhi ya maoni kwenye runinga na redio, napata nguvu ya kuamini kwamba nchi yetu haijaishiwa watu ambao ni jasiri wa kupambana na ufisadi.”

 

Hii ni kauli ya Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, Barnabas Samatta.

 

Mwai Kibaki: Uongozi siyo kujinufaisha binafsi

“Uongozi ni fursa ya kuboresha maisha ya wengine, siyo nafasi ya kujinufaisha binafsi.”

 

Haya yalisemwa na Rais Mwai Kibaki wa Kenya, kuhimiza jukumu na uadilifu wa kiongozi.

 

1315 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!