Nyerere: Mnakimbilia Ikulu kufanya nini?

“Nilipokuwa Dar es Salaam, nilieleza mahali fulani kwamba watu wanaotaka kutuongoza wawe angalau na sifa… Sasa nasema, hata kama wanazo bado tutawauliza: Sifa mnazo, lakini mnakwenda Ikulu pale kufanya nini?”

 

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, katika maadhimisho ya Sikukuu ya Mei Mosi, 1995, mjini Mbeya.

Kawawa: Wanaojilimbikizia mali wahojiwe

“Hatupendi ulimbikizaji mali wa haramu, na hivyo viongozi wote wanaojilimbikizia mali kwa njia hiyo, wafuatiliwe, waulizwe, waseme walizipataje.”

 

Waziri Mkuu wa zamani Tanzania, Rashid Kawawa, aliyasema haya katika mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuzindua kitabu kinachoitwa, “CCM na mustakabali wa nchi yetu”.

 

Anais Nin: Upendo kamwe haufi kiasili

“Upendo kamwe haufi kifo cha asili. Unakufa kwa sababu hatujui kudhibiti chanzo chake. Unakufa kwa upofu, makosa na usaliti…”

 

Haya ni maneno ya Mwandishi maarufu wa majarida, riwaya, tafiti, insha na hadithi wa nchini Ufaransa na Cuba, Anais Nin.

 

Zig Ziglar: Mmezaliwa ili kushinda

“Mmezaliwa ili kushinda, lakini ili kuwa mshindi, lazima kupanga kushinda, kujiandaa kushinda na kutarajia kushinda.”

 

Hii ni kauli ya Mwandishi na mfanyabiashara maarufu wa nchini Marekani, Hilary Hinton anayejulikana zaidi kwa jina la Zig Ziglar.

 

 

By Jamhuri