NUKUU ZA WIKI 68

Nyerere: Tunamtaka rais anayechukia rushwa

“Rushwa ni adui wa haki. Tunamtaka rais atakayelitambua hilo, atakayeichukia rushwa hata ukimuangalia aoneshe kweli anaichukia rushwa, sio rais anayesema kweli rushwa ni adui wa haki…. lakini ukimwangalia usoni unashangaa na kusema…. aaaah kweli huyu?”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kikwete: Hakuna mshindi mgogoro wa kidini

“Kamwe hakuna washindi wa mgogoro wa kidini. Nchi ikisambaratika wote tutapoteza… Kuna mifano mingi juu ya jambo hili.”

Rais Jakaya Kikwete aliyasema haya kukemea uhasama wa kidini nchini.

 

Michelle: Najivunia mabadiliko ya nchi yangu

“Katika maisha yangu ya ukubwa, kwa kweli najivunia nchi yangu. Si tu kwa sababu Barack amefanya vizuri, lakini kwa sababu nadhani watu wana njaa ya mabadiliko. Nimekuwa nikiamani kuona nchi yetu inakwenda katika mwelekeo huo.”

Haya ni mameno ya Michelle Obama, Mke wa Rais Barack Obama wa Marekani.

 

Shakespeare: Penda wote, usimkosee yeyote

“Penda wote, amini wachache, usimkosee yeyote.”

Hii ni kauli ya mtunzi wa mashari na hadithi, na mwandishi maarufu katika lugha ya Kiingereza, William Shakespeare.