Nyerere: Tuwe makini kuchagua viongozi

“Hatari moja ya kuendelea kumchagua mtu yule yule kipindi hata kipindi huweza kuleta hofu na wasiwasi nchini.”

Haya ni maneno ya Baba wa taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Gurdjief: Binadamu huwa anabadilika

“Binadamu hawezi kubaki hivyo alivyo kwa muda mrefu. Kila wakati anabadilika. Ni mara chache anaweza kubaki hivyo alivyo.”

Kauli hii ilitolewa na mwalimu wa kiroho wa nchini Urusi, George Gurdjieff. 

Kabaka: Ajira kwa vijana bado tatizo

“Vijana wengi wanahamia mijini na kuishia kukosa ajira, lakini pia vijana walioko vijijini wanakosa ajira kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo huathiri kilimo.”

Maneno haya ni ya Waziri wa Ajira na Kazi Tanzania, Gaudentia Kabaka.

 

Arinze: Imani ya Katoliki haitabadilika

“Imani ya Kanisa Katoliki haitabadilika kamwe. Lakini lugha na mazingira ya kudhihirisha imani hii vinaweza kubadilika kulingana na watu, nyakati na mahali.”

Hii ni kauli ya kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Nigeria, Kadinali Francis Arinze.

1542 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!