Nyerere: Wafanyakazi wasinyonywe, waheshimiwe

“…wafanyakazi wa Tanzania wamelindwa wasinyonywe na matajiri wao, watu binafsi, na hata mashirika ya umma. Kila mfanyakazi apate heshima yake kama binadamu.”

Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere aliyasema haya kukemea unyonyaji dhidi ya wafanyakazi.

Queen Victoria: Ujauzito humhatarisha mwanamke

“Kuwa mzamzito ni kazi ya hatari ya kuwa mwanamke.”

Kauli hii ni ya Malkia Victoria, aliyekuwa mtawala wa Uingereza na Ireland kuanzia Juni 20, 1837 hadi kifo chake. Alizaliwa Mei 2, 1819, alifariki Januari 22, 1901.

 

Bruce Lee: Bora swali la kipumbavu

“Mtu mwenye busara anaweza kujifunza mengi kutokana na swali la kipumbavu kuliko mpumbavu anavyoweza kujifunza kutokana na jibu la busara.”

Haya ni maneno ya msanii mwigizaji na mtengenezaji wa filamu maarufu duniani raia wa China, Bruce Lee. Alizaliwa Novemba 27, 1940, alifariki Julai 20, 1973.

 

Mubarak: Mchagueni mgombea mnayemtaka

“Nina haya ya kuwambia watu: nendeni kwenye uchaguzi, na mkampigie kura mgombea ambaye ni chaguo lenu. Huu ni wajibu wenu; msiupuuze.”

Maneno haya ni ya Rais Hosni Mubarak wa Misri. Aliiongoza nchi hiyo mwaka 1981 – 2011.

 

3481 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!