Nyerere: Tuchague viongozi wanaostahili

“Ni dhahiri kwamba uongozi wa Chama chetu lazima ushikwe na wanachama wa CCM. Tunachoweza kukosolewa ni kwamba wakati mwingine tunachagua viongozi wasiostahili.”


Haya yalisemwa na Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, wakati akihimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuondokana na kasumba ya kuchagua viongozi wasiostahili.

Child: Imani ya kweli inajenga mafanikio

“Imani katika nafsi ni moja ya matofali muhimu zaidi katika kujenga mradi wowote wa mafanikio.”

 

Hii ni kauli ya mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na mwandishi wa habari wa nchini Marekani, Lydia Child. Alizaliwa Februari 11, 1802 huko Medford, alifariki Oktoba 20, 1880 mjini Wayland.

 

Obasanjo: Binadamu hawezi, Mungu anaweza

“Hisia zangu nzuri na imani yangu vinaniambia kwamba hadi Mungu anafunga mlango, hakuna binadamu awezaye kuufunga.”

 

Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, aliyasema haya wakati akiwakumbusha watu kutambua kwamba lisilowezekana kwa binadamu linawezekana kwa Mungu. Alizaliwa Machi 5, 1937 Abeokuta, Nigeria.

 

Carter: Unaweza kufanya zaidi ya unavyofikiri

“Unaweza kufanya unaloweza kufanya, na wakati mwingine unaweza kulifanya hata zaidi ya unavyofikiri unaweza.”

 

Maneno haya ni ya Rais wa 39 wa Marekani, Jimmy Carter. Alizaliwa Oktoba 1, 1924 mjini Plains, Marekani. Alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2002.

 

1465 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!