“Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache katika nchi yao wenyewe….”

Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, aliyasema hayo kuwahimiza Watanzania kupinga vitendo vya ukandamizaji ndani ya nchi yao.

Gandhi: Tusikatae kusikilizana

“Mabadiliko ya kidemokrasia hayawezekani iwapo hatupo tayari kusikiliza upande mwingine. Tunafunga milango ya kufikiri wakati tunapokataa kuwasikiliza wapinzani wetu, au baada ya kuwasikiliza tunawafanyia mzaha. Kutokuvumiliana kunapokuwa ndio mazoea, tunajiweka katika hatari ya kutokujua ukweli.”

Baba wa Taifa la India, Mahatma Gandhi, aliyasema hayo kusisitiza umuhimu wa wanasiasa kujenga dhana ya kusikilizana na kuvumiliana ili kuleta mabadiliko ya kweli ya kidemokrasia.

Mkapa: Tukabili umaskini

“Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini sana duniani, na sasa tumeazimia kuondokana na aibu hiyo.  Tumebuni Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inayokusudia kutufanya tuwe taifa ambalo watu wake walio wengi watakuwa na maisha bora.”

Rais mstaafu Benjamin Mkapa, aliyasema hayo katika maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi, 2001), akisisitiza umuhimu wa Watanzania kuwa na maisha bora.


Mandela: Jenga amani

“Kama unataka kujenga amani na adui yako, unapaswa kufanya kazi na adui yako. Halafu anakuwa mwenzako.”

Kauli hiyo ni ya Rais mstaafu Nelson Mandela wa Afrika Kusini, wakati akieleza mbinu thabiti ya kujenga amani baina ya maadui.


By Jamhuri