“Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi.  Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha CCM kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao.”

Haya ni maneno ya Mwasisi na Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, wakati akiwahusia viongozi wa CCM kujirekebisha na kutumikia wananchi.

Darwin: Muda ni maisha

 

“Binadamu yeyote anayepoteza saa moja hajagundua thamani ya muda (maishani).”

Maneno haya yalisemwa na mwanasayansi anayeheshimika mno duniani, Mwingereza aliyegundua dhana ya mabadiliko (evolution), Charles Darwin, wakati akisisitiza umuhimu wa kufanya kazi.

Gandhi: Tusikate tamaa

“Ishi kama vile unakufa kesho. Jifunze (mambo mengi) kama vile utaishi milele.”

Hii ni kauli ya mpigania uhuru na Baba wa Taifa la India, Mahatma Gandhi, wakati akiwahamasisha wenzake kujipatia maarifa mengi kadri inavyowezekana bila kujali watakufa lini.

Luther King: Giza hatari

“Giza haliwezi kuondoa giza, bali mwanga unaweza. Chuki haiwezi kuondoa chuki, bali upendo unaweza.”

Haya yalinenwa na mpigania haki za binadamu nchini Marekani, Martin Luther King Jr., alipokuwa akiwahamasisha Wamarekani kupendana badala ya kubaguana.

By Jamhuri