Kocha wa Mabingwa Ligi Kuu Uingereza, Pep Guardiola ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu England kufuatia kuiwezesha Manchester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini humo na kuwashinda Makocha wenzake walikuwepo kwenye Kinyang’anyiro hicho ambao ni Roy Hogson wa Crystal Palace, Jurgen Klopp wa Liverpool, Chris Hughton wa Brighton, Rafael Benitez wa Newcastle United na Sean Dyche wa Burnley.

Guardiola ameisaidia City kufikisha pointi 100 msimu huu pamoja na kushinda jumla ya mechi 32 huku akipoteza michezo miwili pekee.

Mbali na ushindi huo, kikosi chake kimeweza kufunga jumla ya mabao 106 na kikiweza kwenda sare katika michezo minne.

Guardiola alijiunga na Manchester City msimu wa 2016/17 akitokea Bayern Munich inayoshiriki ligi ya Bundesliga.

By Jamhuri