Peter Msigwa Asema Wabunge wa CCM Wanampaka Mafuta kwa Mgongo wa Chupa Rais Magufuli

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, akichangia hoja katika mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya serikali 2018 / 2019 iliyowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango, amemvaa waziri huyo wa fedha, na kumwambia kwamba alipoanza kuhutubia alianza kwa nadharia, na hakusikiliza kuhusu kodi ambazo ametoa zingeleta matatizo kwenye uchumi hakusikiliza.

Mh. Msigwa amesisitiza kuwa utaratibu wa muelekeo wa uchumi unaoendelea sio halisia, na kusema kuwa wao wanaoongea ndio wanaombea rais wa jamhuri kwasababu kuliko wengi ndani ya bunge sabau wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa, na kuendelea kusema kuwa uchumi haukuwi.

Vilevile amesema kuwa serikali ya wamu ya tano inaendesha nchi kama sudan ya kusini, amesema kuwa tangu nchi imepatikana imeendeshwa na cha cha CCM pekee, Hayati nyerere watamsamehe sabau nchi ndio ilikuwa inaanza ambapo amewataja viongozi wengine kwa mazuri walioyafanya akiwemo rais Mwinyi, Mkapa na Kikwete, swali zito amemuuliza kuwa Mh Mpango kuwa wakati wa rais Kikwete Waziri huyo alisimamia gesi, PPP, Standard Gage. na kutaka Waziri Mpango aiambie Bunge kuwa yeye ni mchumi anaeamini nini.

Hata hivyo ametaka atofautishe uchumi uliokuwa kipindi cha Kikwete, ambao ulitengeneza mazingira mazuri ulikuwa na makosa au alimuingiza chaka, na sasa hivi amebadilika kutokana na uchumi wa awamu ya tano ambao unagombana na wawekezaji wanaonekana wote wezi na kutolipa kodi na athibitishe uchumi anaoamini, na amtaje rais anaemdanganya Rais wa awamu ya tano au Rais wa awamu ya nne.