Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limewahakikishia usalama wageni wote wanaotarajia kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru, Disemba 9 na kuwataka kuwa na amani kwani Jeshi hilo limejipanga kikamilifu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatatu, Disemba 4, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto ameeleza kuwa jeshi la polisi limejipanga kufanya misako ya aina zote ili kuhakikisha kuwa wanawabaini wahalifu wanaojipenyeza katikati ya raia wema.

Kamanda Muroto alitoa onyo kwa wale wote waliojipanga kufanya uhalifu waache mara moja kwani watashughulikiwa ipasavyo.

 

 

 

 

 

1537 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!