Power on Fitness Gym iliyopo Mwenge, kinondoni, Jijini Dar es salaam imeandaa siku maalumu kwa ajili ya kujumuika pamoja, kufanya mazoezi na kuukaribisha mwaka mpya wa 2018.

Shughuli hiyo itafanyika siku ya jumamosi January 27,2018 katika viwanja vya posta vilivyopo Sayansi, Kijitonyama. Shughuli hii itanzaa saa 12 asubuhi mpaka usiku.

Siku hiyo kutakuwa na mazoezi ya kukimbia(Jogging) ambayo itaanza alfajiri ya saa 12, na kufuatiwa na mazoezi ya Aerobics, Steps, Zumba, Mpira wa miguu, na michezo mingine kama kuvuta Kamba, Kukimbiza Kuku nk.

Baada ya mazoezi, kutakuwa na burudani kabambe ya muziki itakayoongozwa na bendi ya Skylight bila kusahau burudani ya muziki itakayoporomoshwa na Ma DJ wakali wa hapa nchini.

Siku hiyo pia kutakuwa na Nyama choma itakayoandaliwa kiufundi na wapishi waliobobea, Supu bila kusahau vinywaji vya kila aina.

Wadahamini wa shughuli hiyo ni Kampuni ya JSP Marketing Link Limited ikishirikiana na Msouth Company, Dagaa Microfinance Limited, Simba Makini Group, Jaina Ice Cubes, Micgen Insurance Brokers, TTCL na wenyeji Power on Fitness Gym.

Mwisho.

2753 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!