Gareth Bale

Real Madrid ya Hispania usiku huu wamefanikiwa kunyakua taji la Klabu Bingwa Ulaya baada ya kuwalaza Liverpool kwa mabao 3-1.

Awali mchezo huo, ulikuwa wa kasi na kuvutia, ambapo dakika 45 za kipindi cha kwanza milango ilikuwa migumu na matokeo yalikuwa 0-0.

Katika kipindi cha pili Real Madrid walijipatia bao lao la kwanza la kuongoza kupitia kwa Karim Benzema alifunga bao kutokana na uzembe wa Goli kipa wa Liverpool kumgongesha mpira na kuingia golini kwake  katika dakika ya 53 na bao hilo lilidumu kwa dakika 3 kabla ya Sadio Mane kuisawazishia Liverpool katika dakika ya 55.

Baada ya Liverpool kusawazisha bao hilo Real Madrid walikuja juu na kulisakama lango la Liverpool katika dakika ya 64 Gareth Bale alifunga bao la pili na dakika ya 83 Gareth Bale tena aliihakikishia ushindi Madrid kwa kupachika tena bao la tatu

Hadi dakika 9o, zinamalizika ubao unasomeka Madrid  3-1 liverpool.

2805 Total Views 4 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!