Rooney Atimka Everton, Akimbilia Marekani

Aliyekuwa mshambuliaji wa Everton, Wayne Rooney (32) amesaini kandarasi ya miaka mitatu na nusu kuitumikia Klabu ya DC United inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Marekani.

Rooney ambaye atakamilisha uhamisho wake huo wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa Julai 10 mwaka huu, atalipwa mkwanja kiasi cha Pauini Milioni 10 (sawa na Tsh. Bilioni 26.47) ambapo atakuwa ni mchezaji mwenye kulipwa pesa ndefu zaidi nchini Marekani.

Rooney ambaye anashikilia rekodi ya mfungaji Bora wa muda wote wa Manchester United na Uingereza amekatisha mkataba wake wa miaka miwili aliosaini mwaka jana kuitumikia Everton..

Staa huyo ambaye pia ni mfungaji Bora wa Pili wa Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na mabao 208 nyuma ya kinara Alan Shearer aliyekuwa na mabao 260, anatengengeneza rekodi nyingine ya kuungana na mastaa kibao wa soka waliowahi kutoka Uingereza na kwenda kucheza soka la kulipwa Marenaki.

Miongoni mwao ni David Beckham, Thierry Henry, David Villa, Steven Gerrard, Didier Drogba, Andrea Pirlo Zlatan na Ibrahimovic.

 

2016 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!
Tags :
Show Buttons
Hide Buttons