Mwanasoka wa kimataifa wa nchini Uingereza, Wayne Rooney, anayechezea klabu ya Manchester United, anatarajiwa kuongoza kikosi cha England dhidi ya San Marino katika mtanange wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Brazil, mwaka 2014.

Rooney (26), ameteuliwa kuongoza kikosi hicho baaada ya nahodha mkuu, Steven Gerald, kusimamishwa katika michezo kadhaa na nahodha msaidizi, Frank Lampard, kutoweza kushuka dimbani kutokana na majeraha yanayomkabili.


Nguli huyo wa soka amewaahidi wachezaji wenzake na mashabiki wake kuwa hatorudia makosa yaliyokwamisha jitihada zake katika fainali za EURO kwa mwaka 2012, baada ya kupata adhabu ya kutoshuka dimbani katika michezo miwili mfululizo ya kimataifa.


Mshambuliaji huyo alikosa mechi kati ya Ufaransa na Sweden baada ya kupewa kadi nyekundu.

1033 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!