Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na Yanga utakaochezwa leo Jumapili  29,2018 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam,

utakuwa mgumu Zaidi ya chuma kutokana na historia ya timu hzio zinapokutana huwa ni vigumu kutabiri.

Lakini katika mchezo wa leo Simba inapewa nafasi kubwa ya kushinda kuliko Yanga kwani Simba msimu huu inaonekana ipo vizuri na haijapoteza hata mchezo mmoja kwa hiyo itaitaji kutunza record yake na kujiweka karibu kuchukua ubingwa, kwani dhairi kama kweli leo Simba atashinda basi nafasi ya Yanga kutetea ubingwa itakuwa imepotea.

Ndugu Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye Uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo huo namba 178 utakaoanza saa 10 jioni.
Tayari tiketi za mchezo huo zinaendelea kuuzwa ambapo VIP A ni shilingi 30,000,VIP B na C 20,000 na Mzunguko (Jukwaa la rangi ya Chungwa, Kijani na Bluu) 7,000.
Tiketi zinapatikana kupitia Selcom.

Vikosi Vinavyotarajia kuanza leo

 

Simb SC

Aishi Manula, Nicholas Gyan, Erasto Nyoni, Yusuph Mlipili, Juuko Murshid, Asante Kwasi, Jonas Mkude, Shomari Kampombe, Shiza Kichuya, John Bocco, Emmanuel Okwi

 

Yanga SC

Youthe Rostand, Hassan Kessy, Vicent Andrew, Kelvin Yondani, Gadiel Michale, Juma Said, Papy Tshishimbi, Pius Buswita, Yusuph Mhilu, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib

12179 Total Views 2 Views Today
||||| 5 I Like It! |||||
Sambaza!