Staa wa timu ya taifa ya England anayecheza club ya Man City inayoshiriki Ligi Kuu England Raheem Sterling baada ya headlines za muda mrefu na watu kuhoji kwa tattoo yake ya bunduki mguuni ameamua kufunguka.

Raheem Sterling ambaye ni raia wa England mwenye asili ya Jamaica, ameeleza sababu pekee iliyomfanya achore tattoo ya bunduki katika mguu wake wa kulia ni kutokana na kiapo chake alichojiwekea kuwa hatokuja kushika bunduki katika maisha yake kutokana na baba yake mzazi aliuuwawa na bunduki wakati yeye akiwa na umri wa miaka miwili.

Kama hufahamu Sterling alizaliwa mwaka 1994 nchini Jamaica katika mji wa Kingston wilaya ya Maverley, alihama Jamaica na mama yake na  kwenda London England akiwa na umri wa miaka mitano, hiyo ikiwa imepita miaka mitatu toka baba yake mzazi auwawe.

Yametimia maneno ya mchambuzi mkongwe Dr Leaky kuhusu Champions League

1106 Total Views 5 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!