Tag Archives: Dk. John Magufuli

Rais Magufuli Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere

Rais Dkt. Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwl. Julius Nyerere kilichopo Kibaha, Pwani. Chuo hicho kinajengwa kwa gharama ya Sh. Bil 100, kwa ufadhili kutoka chama cha CPC cha China kwa ajili ya vyama 6 vya ukombozi Africa (CCM, ANC, ZANU-PF, Frelimo, MPLA na SWAPO na kitachukuwa miaka miwili mpaka kukamilika kwa ujenzi. ...

Read More »

RAIS DK. MAGUFULI ATENGUA NA KUTEUA MKURUGENZI MKUU NSSF

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Prof. Godius Kahyarara kuanzia leo 14 July 14, 2018. Prof. Kahyarara atapangiwa kazi nyingine. Kufuatia hatua hiyo, Rais Magufuli amemteua William Erio kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF. Kabla ya uteuzi huo Erio alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa ...

Read More »

JINSI RAIS MAGUFULI ALIVYOFANYA ZIARA YA GHAFLA BANDARINI DAR ES SALAAM KUKAGUA MATANKI YA MAFUTA YA KULA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa ...

Read More »

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA VIJIJI MBALIMBALI VILIVYOPO KILOMBERO WAKATI AKIWA NJIANI KUELEKEA KUFUNGUA DARAJA KUBWA LA MTO KILOMBERO LILOLOPEWA JINA NA DARAJA LA MAGUFULI

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mang’ula kona katika Wilaya ya Kilombero wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli lenye urefu wa M384) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe ...

Read More »

MAGUFULI: Mradi wa Ujenzi wa Ukumbi wa Mihadhara MUCE lazima Kichunguzwe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameviagiza vyombo vya dola, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuchunguza mradi wa ujenzi wa jengo la ukumbi wa mihadhara na ofisi za Wahadhiri katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kilichopo katika Manispaa ya Iringa. Mhe. Rais Magufuli ...

Read More »

Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais

Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli. Mimi ambaye ni mkazi wa Mkoa wa Tabora niliporwa nyumba yangu mwaka 2006 na wenye uwezo wa kiuchumi lakini mpaka leo sijafanikiwa kuipata. Kwamba mheshimiwa rais, nilijitahidi kufuata hatua zote muhimu zikiwa ni pamoja na za kijamii na za kisheria ndani ya mkoa huu ilishindikana. Kwamba mheshimiwa rais, kutokana na hali ya mambo kuwa kama ...

Read More »

Israel Yampongeza Rais Magufuli

Serikali ya Israel imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kurejesha uhusiano unaolenga kuziimarisha nchi hizi mbili kiuchumi. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Ayelet Shaked wakati wa Kongamano la Tano la Biashara na Uwekezaji kati ya Israel na Tanzania. “Tunamshukuru sana Rais Magufuli kwa ...

Read More »

Rais Dkt Magufuli afanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPB

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Edmund Bernard Mndolwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB). Uteuzi wa Dkt. Mndolwa umeanza leo tarehe 23 Aprili, 2018. Dkt. Mndolwa anachukua nafasi ya Prof. Lettice Rutashobya ambaye amemaliza muda wake. Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dodoma ...

Read More »

Hongera Rais John Magufuli

Wiki iliyopita, Rais John Magufuli alipokea ndege aina ya Bombardier Q400 yenye uwezo wa kubeba abiria 70, ikitokea nchini Canada. Katika hafla hiyo, Rais Magufuli akawataka Watanzania kujivunia ndege hiyo ya tatu ikiwa ni miongoni mwa ndege sita alizoahi kuzinunua. Pia Rais Magufuli alizindua ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 uliojengwa kuzunguka eneo lenye madini ya Tanzanite lililopo Mirerani mkoani ...

Read More »

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA KUMSIMIKA MHASHAMU ISAAC AMANI KUWA ASKOFU MKUU JIMBO KUU KATOLIKI LA ARUSHA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Askofu Msaidizi Prosper Lyimo  alipowasili kushiriki Ibada ya Kumsimika Mhashamu Isaac Amani kuwa Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki  Arusha katika Kanisa la Mtakatifu Theresia la Mtoto Yesu Jimbo Kuu Katoliki jijini Arusha leo Aprili 8, 2018   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ...

Read More »

Mikutano hii iwe ya mara kwa mara

Wiki iliyopita, Rais John Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa sekta mbalimbali nchini. Masuala mengi yalizungumzwa na wafanyabiashara wenyewe, tofauti na ilivyozoeleka ambako kazi hiyo ilifanywa kwa uwakilishi. Waliopata nafasi walizungumza matatizo yanayowakabili na wakatoa mapendekezo ya kutatua kero mbalimbali. Tunampongeza Rais Magufuli na Serikali kwa jumla, kwa kuwa wasikivu. Hata hivyo, mkutano huo unaweza usiwe na tija ...

Read More »

Hongera JPM kwa uamuzi huu

Wiki mbili zilizopita Mpita Njia (MN) akiwa kwenye gari linalofanya kazi ya kusafirisha abiria (Heace)  kati ya Muganza na Buselesele Wilayani Chato, Mkoani Geita,  aliwasikia abiria  watatu wakiteta juu ya uteketezaji wa nyavu na ukamataji wa wavuvi haramu unaoendelea katika ziwa victoria. MN alivutiwa na mazungumzo ya abiria hao kwani walionekana kuwa na mitazamo tofauti  katika mzungumzo yao. Katika mazungumzo ...

Read More »

Magufuli Awanyooshea Kidole Wanaotaka Kuandamana

Rais Dkt John Magufuli amewaonya vikali watu wanaopanga kufanya maandamano nchini humo akisema kwamba hawataruhusiwa. “Wapo watu wangependa nchi hii kila siku tuwe na migogoro,” amesema Dkt Magufuli. “Wapo watu ambao wameshindwa kufanya siasa za kweli, wangependa kila siku tuko barabarani tunaandamana. Watu wao wanahamia huku, wao wanataka wabaki wanaandamana kule. Nitasema ngoja waandamane wataniona. Kama kuna baba zao wanawatuma, ...

Read More »

Ndugu Rais, amani kwanza mengine tutayapata kwa ziada

Ndugu Rais, lengo la maandiko yetu siku zote siyo kukosoa. Udhaifu wa kuandika kwa sababu unampenda mtu au unamchukia mtu, Mwenyezi Mungu katuepusha nao. Hatuandiki kwa ushabiki wa kumshabikia mtu au chama fulani. Wala hatuandiki hapa kwa lengo la kusifia au kupongeza. Tunaandika kile ambacho tunaamini kuwa ni ukweli mtupu, kwa lengo la kushauri tu. Tunaamini kuwa kwa hizi busara ...

Read More »

JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI ZAIPAISHA TANZANIA, DHIDI YA MAPAMBANO YA RUSHWA

Juhudi thabiti ya Rais John Pombe Magufuli katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya Taifa imezidi kuleta mafanikio ambapo ripoti mpya katika mapambano dhidi ya rushwa imeonesha Rwanda na Tanzania kuongoza katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika mapambano dhidi ya rushwa kwa mwaka 2017. Kwa mujibu wa Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Rushwa (Corruption Perception Index) iliyotolewa ...

Read More »

KUFUATIA KIFO CHA MWANAFUNZI WA NIT, RAIS MAGUFULI ATOA AGIZO

Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia ya Akwilina Akwilini aliyeuawa baada ya kupigwa na risasi katika maandamano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Februari 16, 2017 eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam Katika salamu hizo, Rais Dkt Magufuli amesema kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho ...

Read More »

RAIS MAGUFULI AWATAKA VIONGOZI WA DINI NA WAUMINI WAO WASIJIHUSISHE NA MIGOGORO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi na waumini wa madhehebu ya dini nchini kujiepusha na migogoro ambayo imekuwa ikiharibu sifa na heshima ya taasisi hizo muhimu katika jamii. Mhe. Rais Magufuli ametoa wito huo leo tarehe 04 Februari, 2018 mara baada ya kuhudhuria Ibada ya kuwekwa wakfu kwa Askofu wa Tano wa ...

Read More »

Rais Magufuli Akutana na Dkt. Slaa Ikulu

Rais Magufuli akifurahia jambo na Dkt. Slaa.   RAIS Dkt. John Magufuli amempongeza Balozi mteule Dkt. Wilbrod Slaa kwa moyo wake wa kizalendo wa kukubali kwenda kuiwakilisha nchi ya Tanzania katika taifa ambalo atapangiwa muda wowote kutoka sasa huku akijivunia kuwa hakukosea kumchagua yeye (Dkt Slaa) Magufuli akiagana na Slaa.   Rais Magufuli ameeleza hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo ...

Read More »

NDUGU RAIS NAKUPONGEZA HATA KAMA HAWAPENDI

Ndugu Rais, nakupongeza kwa kuwaumbua akina ‘Grace’ wetu wanaokupigia chapuo uongezewe miaka ya urais. Wangekuwa ni watu wa kuona aibu wangetafuta mahali pa kuzificha sura zao. Lakini wauza utu sawa na wauza miili. Aibu waipate wapi? Kama Mugabe angempuuza Grace wake kama ulivyowapuuza hawa ‘Grace’ wetu, nina hakika Robert Mugabe angekuwa bado ni Rais wa Zimbabwe. Siyo kwamba wana mapenzi ...

Read More »

RAIS MAGUFULI APIGA MARUFUKU WANAFUNZI KURUDISHWA NYUMBANI KWA KUKOSA MICHANGO ILIYO NJE YA KARO ZA SHULE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 17, 2018 amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za Serikali za msingi na Sekondari na kuwaagiza Mawaziri Jafo na Ndalichako kusimamia hilo. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo mara baada ya kufanya kikao na waziri wa TAMISEMI Suleiman Jaffo na waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako ...

Read More »

Rais Magufuli Aomboleza Vifo vya watu 11 Kagera

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kufuatia watu 11 kupoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Nyangozi, Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera. Ajali hii imetokea jana tarehe 14 Januari, 2018 majira ya saa 11 jioni baada ya ...

Read More »

Barua ya Wana Moshi kwa Rais John Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli, barua yetu inahusu BOMOA BOMOA YA RAHCO KATIKA ENEO LA PASUA BLOCK JJJ ILIYOSABABISHWA NA MGONGANO WA MAMLAKA MBILI ZA SERIKALI. Mheshimiwa Rais, kwanza tunapenda tuchukue fursa hii adimu, kukupongeza kwa dhati kabisa kwa kuchaguliwa kwako kuliongoza Taifa la Tanzania, na tunathubutu kusema, hakika tulichelewa sana kupata Rais ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons