Mwenyekiti wa Tahlisi George Albert  Mnali  wa pili kutoka kulia akizungumza na baraza Kuu la Senate leo  kushoto ni Katibu Mkuu wa Tahliso John Mboya kulia ni Katibu wa Baraza hilo Faidhaa Msangi na kulia ni Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Rais wa Chuo cha Zanzibar University  

JUMUIYA YA TAASISI ZA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA

(TAHLISO)OFISI YA MWENYEKITI TAHLISO

TAARIFA KWA UMMA.

Ndugu waandishi wahabari tunawashukuru sana kwa kukubali wito wetu wa kuja kujumuika pamoja na sisi. Leo tarehe 3/3/2018 (Jana) tumekutana viongozi wa vyuo vikuu nchi nzima kwa ajili yakujadili changamoto zinazotukabili. Kikao hiki ni cha TAHLISO BarazaKuu (SENATE) kinacho husisha Maraisi wa serikali za wanafunzi wa VyuoVikuu nchini.

Tunatambua kwamba kuna kifo cha mwanafunzi mwenzetu Akwilina Akwilini,mwanafunzi wa chuo cha NIT kilichotokea mwezi wa pili. Tunawashukuru wanafunzi wenzetu kwa utulivu mkubwa na mshikamano waliouonesha tangu msiba ulipotokea, wakati wa kipindi cha majonzi hadi kufikia sasa.

Tunamshukuru Mhe.Raisi wa Jamuhuri ya Muunganowa Tanzania kwa kuingilia kati suala hili na kuagiza uchunguzi ufanyike na hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote watakaobainika kuhusika na kifo cha Akwilina Akwilini.

Vilevile tunaishukuru Wizaraya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ukaribu waliouonesha katika kipindi chote cha msiba.Tunaomba wanafunzi waendelee kuwa watulivu wakati maagizo ya Mh. Raisi yakitekelezwa.

Aidha tunapenda jamiii itambue kuwa TAHLISO ndio chombo kikuu cha kuwasemea wanafunzi wote nchi nzima Tanzania na sio kikundi kingine chochote kile.

Vipo vikundi vingi vimejitokeza na kutoa matamko mbalimbali baada ya kifo hiki kutokea, vikundi vingine vikaenda mbali Zaidi kwa kuwataka baadhiya watendaji wa Serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani kujiuzulu jambo ambalo linaashiria vikundi hivyo kuongozwa ama kutumika namakundi ya kisiasa, haiwezekani kutaka watendajiwa Serikali wajiuzulu wakati uchunguzi bado unafanyika na matokeo ya uchunguzi huo bado hayajatoka.

Sehemu ya Marais wa Vyuo Vikuu nchini wakiwa kwenye mkutano huo

Jambo la kusikitisha Zaidi kuna baadhi ya vikundi vimejitangaza kwamba vinaungwa mkono na Maraisi wa Vyuo Vikuu jambo ambalo sio la kweli, Marais wote wa Vyuo Vikuu tuko hapa Dodoma tunaendelea na vikao vyetu vya kujadili changamoto zinazowakabili wanafunziwa VyuoVikuu.

Tunatoa wito kwa vikundi vyote vinavyojihusisha nakutumia mwamvuli wa Marais waVyuoVikuu kama kinga yao ili kuu hadaa Umma kwamba wanaungwa Mkono, vikundi hivyo viache tabia hiyo vinginevyo tutawachukulia hatua za kinidhamu.

TAHLISO tunasubiri matokeo ya Uchunguzi unaofanyika juu ya kifo cha Akwilina na tunaimani wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Tunawaomba wanafunzi wote tuendelee kuwa watulivu wakati tukisubiri matokeo hayo na kujiepusha na maandamano na vitendo vyovyote vitakavyo sababisha uvunjifu wa Amani nakuleta mgawanyo miongoni mwa wanafunzi.

Hata hivyo namna bora yakufikisha hoja nikutumia njia ya majadiliano kama wasomi badala ya kutumia nguvu ama maandamano kwa kutofuata taratibu na madhara yake ni kusababisha vuruguzi sizotakiwa na hatimaye kuhatarisha usalama na hivyo kuathiri jamii kwaujumla wake.

Vurugu zozote zitokanazo kwa kutozingatia taratibu zinaweza kudhorotesha shughuli za kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Uchumiwa Taifa letu. Vile vile zinapoteza mvuto kwa wawekezaji wanje na wandani, ikiwemo shughuli za utalii nchini ambazo zinachangia pato la Taifa letu.

Athari za Vurugu na kukosekana kwa amani zipo wazi natunaziona kwa nchi nyingine zikiwemo baadhi ya nchi jirani zetu ambao wamekua wakimbizi nchini kwetu kila siku.

Tunaona kuwa kama wanataaluma tunajukumu kubwa la kuelimisha jamii na kuwamfano bora wakutumia njia za majadiliano katika kujenga hoja zetu ilizitatuliwe kuliko kutumia njia ya maandamano au vurugu zisizo na ulazima wowote.
Taasisi hii ndio yenye dhamana ya kutetea nakusimamia maslahi ya wanafunzi wote wa vyuo na vyuo vikuu Tanzania na si vinginevyo.

………………………………….

GEORGE ALBERT MNALI

MWENYEKITI TAHLISO

By Jamhuri