Mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imewafikisha mahakamani watu 13 wakikabiliwa na mashtaka matano ikiwamo ya kusambaza taarifa za uongo, uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha wa zaidi ya Sh154 milioni.

Wakili wa Serikali Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Tumain Kweka amewasomea kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 58 ya 2018 leo Agosti 7mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina.

Amedai kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka moja la kula njama, kuchapisha taarifa za uongo na mawili ya kusambaza taarifa za uongo na shtaka moja la utakatishaji wa fedha.

Kweka aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Boniface Maombe, David Luvanda, Moshi Sungura, Amos Bosco, Lule Kadenge, Jofrey Kapangamwaka, William Nturo, Regius Mauka, Collins Mwang’omolan Francis Kapalata, Kasonde Kapela, Enock Mwandaji na Pascal Kiatu

890 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!