Mchezaji bora zaidi wa Kriketi nchini India mwishoni mwa wiki, ameaga  rasmi mchezo huo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 anatarajia kumenyana na West Indies katika mchuano wa mwisho wa mashindano ya yajulikanayo kama ,Test,  katika uwanja mashuhuri wa Wankhede.

Huu ndio uwanja ambao mwaka 2011, Tendulkar alijionesha kwa dunia kama mchezaji mashuhuri na hivyo nyota yake kuwakia hapo katika maisha yake kama mchezaji wa Kriketi kwa zaidi ya miaka 20 katika Kombe la Dunia la Kriketi.

Kwa mtu anayeshikilia rekodi ya kupata mikimbio mingi zaidi kwenye mchezo huo na kushinda Kombe la Dunia yamekuwa mafanikio na matarajio yake kama mchezaji muda huo wote.

 

Lakini ushindi huu ulikuwa jambo tofauti kwake kwa sababu alishinda kombe nyumbani kwao, nchini India.

 

Awali, alizoea kucheza Soka na Tennis, baadaye alipelekwa na kakake katika uwanja maarufu wa kufanyia mazoezi ya Kriketi, wa Shivaji Park, akiwa na umri wa miaka 11 . Hakuwahi kamwe kujutia kwani hayo ndio yamekuwa maisha yake tangu hapo.


Alivunja rekodi zote katika michuano yote iliyofanyika nyumbani akiwa tu na umri wa miaka 16, alianza kuchezea timu ya taifa.

 

Amekuwa mchezaji ambaye kila mara alikuwa na uwezo wa kutengeneza mikimbio mingi zaidi, alicheza kwa zaidi ya miaka 24 na kucheza mechi yake ya miambili.


Bodi ya kriketi ya India ambayo ndiyo ina fedha nyingi zaidi kuliko zote duniani, ina mipango mizuri kwa mchezaji huyo mashuhuri zaidi kuliko wote. Amepata tiketi 400 kwa mechi hii ya mwisho. Jamaa zake wote wanatarajiwa kufika katika mechi hiyo kumuona akicheza kwa mara yake ya mwisho.


Mama yake anayeugua na anatumia kiti cha magurudumu, atakuwepo katika ukumbi wa wageni mashuhuri kumuona mwanawe akicheza kwa mara ya mwisho.


Kocha wake Ramakant Achrekar pia atakuwepo. Tiketi za kushudia mechi hiyo zenye picha yake, pia zimechapishwa lakini baadhi ya  watu wamekosoa namna zilivyouzwa.


Wapenzi wa Kriketi mjini Mumbai, hawajafurahia sana kwani theluthi mbili ya viti vya uwanja huo, vitatutumiwa na watu ambao hawakununua tiketi.


Wenye maduka mjini Mumbai, wanasubiri mauzo mengi, ya vifaa vilivyo na picha za mchezaji huyo huku vyumba vya kila hoteli iliyo kusini mwa Mumbai vikiwa vimekodiwa.

Mashabiki wa Kriketi nchini India, humtaja mchezaji huyo kama bingwa wa kriketi. Hata hivyo kuna mjadala kuhusu ikiwa yeye ndiye mchezaji bora zaidi wa kriketi duniani.

1220 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!