Tetesi za usajili Ulaya

Baada ya kukamilika kwa usajili wa Neymar kutoka Barcelona kwenda PSG, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Javier Pastore, amempa Neymar  jezi  namba 10 akisema ni shukrani yake kwake ajisikie kuwa nyumbani (tovuti ya PSG).

Naye Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane, anaamini kuwa klabu yake lazima imuuze Gareth Bale (28), kama inataka kumsajili Kylian Mbappe, mwenye umri wa miaka 18, kutoka Monaco (Marca).
Klabu ya Manchester United ya Uingereza wanafuatilia kwa umakini hali ilivyo Real Madrid kama wanaweza kupata nafasi ya kupanda wakapanda dau la pauni milioni 90 ili kumsajili Gareth Bale (Daily Star).
Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa (28), anatarajia kuangalia uwezekano wa kuwasilisha maombi ya kisheria ya kutaka kuondoka katika klabu yake ya Chelsea, baada ya kuambiwa na kocha wake kuwa hayupo katika mipango yake. (independent).

Wakili wa Diego Costa ametishia kuchukua hatua hizo dhidi ya Chelsea baada ya klabu hiyo kupinga Costa kwenda AC Milan kwa mkopo kabla ya kwenda Atletico Madrid mwezi Januari. (Mirror).
Kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard (26), amewasiliana na Barcelona kuhusu kwenda kuziba pengo la Neymar (Don Balon), aliyeondoka klabuni hapo kwa kuweka rekodi ya usajili wa dunia.
Chelsea wapo tayari kupambana na Liverpool katika kutaka kumsajili beki wa kati wa Southampton, Virjil van Dijk (26), kwa kutoa pauni milioni 50 ili kuimarisha kikosi hicho kabla ya kuanza kwa ligi (The Times).
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amekuwa na mawasiliano ya karibu na mchezaji Kylian Mbappe (18), wa Klabu ya Monaco huku benchi la ufundi la timu hiyo ikiendelea kumfuatilia mshambuliaji huyo kwa karibu.

Meneja wa Everton, Ronald Koeman, bado ana matumaini ya kusajili mshambuliaji mwingine, wakati klabu hiyo ikiendelea na juhudi za kumpata mshambuliaji wa Asernal, Olivier Giroud (30) (Liverpool Echo).
Mabingwa wa Ufaransa, Monaco, wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 45 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez (28), ambaye amekuwa katika msuguano na klabu yake kwa muda mrefu (Sun).
Klabu ya Borussia Dortmund wapo tayari kuzungumzia uhamisho wa Ousmane Dembele (20), kwenda katika Klabu ya Barcelona, ikiwa tu Barca watakuwa tayari kutoa euro milioni 100. (Bild) kwa ajili ya Mfaransa huyo.
Kiungo wa Bayern Munich, Arturo Vidal, anataka kurejea Italy, baada ya kufikia makubaliano na Inter Milan ambayo imekuwa katika mawindo ya muda mrefu ya kuhakikisha kiungo huyo mtukutu, raia wa Chile, anarejea (FC InterNews).