kutoka kushoto ni Bw. Patrick Simonnet, mke wangu Alicia, Mkuu wa Desk la Tanzania katika EU, Bi Marta Szilagyi, Tundu Lissu, Bi. Hortensia May Lyatuu na Bi. Vania, ambaye ni afisa wa Ubalozi wa EU Tanzania anayeshughulikia masuala ya utawala bora na haki za binadamu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema jana alitembeleawa na Maofisa watatu kutoka Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa ajili ya kumjulia hali na kuzungumza naye juu ya masuala mbali mbali yanayoihusu Tanzania.

Tundu Lissu amesema kuwa Ujumbe wa EU umeongozwa na Mkuu wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki katika Wizara ya Nje ya EU, Bw. Patrick Simonnet.

Ali ya Tundu Lissu inaendelea vizuri na tunamuombea kwa Mungu azidi kutenda miujiza apone haraka. arudi nyumbani aendelee na majukumu yake kwa wananchi wa Singida Mashariki na Watanzania wote.

4013 Total Views 2 Views Today
||||| 1 I Like It! |||||
Sambaza!